Listra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Paulo na Mt. Barnaba kuko Listra, mchoro wa Willem de Poorter, 1636.

Listra (kwa Kigiriki: Λύστρα, Lyustra) ulikuwa mji wa rasi ya Anatolia, katika Uturuki wa leo.

Kwa sasa ni kijiji tu kinachoitwa Klistra, km 30 kusini kwa Konya[1].

Mji huo unatajwa mara sita katika Biblia ya Kikristo (Mdo 14:6,8,21; 16:1, 2Tim 3:11) kwa sababu kuanzia mwaka 46 Mtume Paulo alifika huko mara kadhaa kuinjilisha akiwa mara na Barnaba, mara na Sila[2]. Ndipo alipomkuta Timotheo ambaye akawa mshirika na hatimaye mwandamizi wake.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kilistra (Gökyurt) Kültür ve Turizm Derneği". kilistra.org.tr.
  2. "Apostle Paul's Second Missionary Journey Map". biblestudy.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-22.

Viungo vyanje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Listra kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.