Tuzo ya Noma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tuzo ya Noma (kwa Kiingereza hujulikana kama Noma Award for Publishing in Africa na kwa Kifaransa hujulikana kama Le Prix Noma de Publication en Afrique) ni tuzo zilizoanza kutolewa mwaka 1980 na kuendelea hadi mwaka 2009. Zilikuwa tuzo za mwaka zenye kuambatana na kiasi cha dola 10,000 kwa kutambua michango ya waandishi wa Afrika. Tuzo hizo zilikuwa kati ya tuzo kubwa kabisa katika bara la Afrika.[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tuzo hii ilianzishwa mwaka 1979 na Shoichi Noma (aliyefariki mwaka 1984), rais wa Kodansha ltd, kampuni kubwa ya uchapishaji nchini Japani.

Tuzo hii ilikuwa na malengo ya kuwatia motisha waandishi wa Afrika[2] na ilikuwa ikitolewa kwa vitabu vipya vilivyokuwa vikichapishwa kila mwaka zikilenga sehemu tatu: uandishi wa fasihi, vijana na wasomi, huku zikidhaminiwa na Kodansha Ltd. Vitabu vilikuwa vilikubaliwa katika lugha yoyote.

Tuzo zilikoma mwaka 2009 baada ya familia ya Noma kusitisha udhamini [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Meena Khorana, mhr. (1998). "Award-winning Children's Books: The Noma Selections, 1980–1994". Critical Perspectives on Postcolonial African Children's and Young Adult Literature. Greenwood Publishing Group. ku. 27–44. ISBN 978-0-313-29864-6. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Oyekan Owomoyela, mhr. (2008). The Columbia Guide to West African Literature in English Since 1945. Columbia University Press. uk. 132. ISBN 978-0-231-12686-1. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "The Noma Award for Publishing in Africa". Noma Award. 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Desemba 2012. Iliwekwa mnamo 18 Mei 2013. {{cite web}}: More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tuzo ya Noma kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.