Omolabake Adenle

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Omolabake Adenle
Amezaliwa 1982
Nigeria
Nchi Nigeria
Kazi yake Mhandisi


Omolabake Adenle (alizaliwa mwaka 1982) ni mhandisi, mjasiriamali na mwanamikakati ya kifedha nchini Nigeria. Omolabake ndiye mwanzilishi na ofisa mtendaji mkuu (mkurugenzi mtendaji) wa AJA.LA Studios, kampuni ambayo hutoa suluhisho na ufumbuzi wa lugha za asili za kiafrika.[1] Adenle aliwasilisha programu ya "SpeakYoruba App" ya kujifunza kuongea pamoja utamaduni wa kiyoruba kwa ujumla ambayo ilishinda tuzo kwa Utofauti wake, Usawa na Ujumuishaji (DEI) wa sauti za Wanawake (WiN) mnamo mwaka 2021.[2] na iliorodheshwa katika tuzo za African Innovation Foundation kwa Afrika (IPA) mwaka 2017.[3][4] Omolabake Adenle ana shahada ya uzamivu ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza.[1]

Maisha ya Mwanzo[hariri | hariri chanzo]

Adenle alizaliwa na kulelewa katika Jimbo la Lagos, Nigeria.[5]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Adenle ana shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Cambridge ambako alikuwa Mshirika wa Utafiti wa Mafunzo ya Sayansi ya Taifa na Tatu Beta Pi Honours.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 McCormick, Meghan (Machi 11, 2019). "Hey Siri! Could Virtual Assistants Be The Missing Link In Internet Accessibility?". forbes.com. Forbes Women: I celebrate women building high-impact companies in Africa. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "2021 Women in Voice Awards". womeninvoice.org. Women in Voice (WiV). 22 Julai 2021. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Innovation Prize for Africa (IPA) 2017 Awards "Investing in Prosperity" – July 17-18, Accra, Ghana". africaninnovation.org. Africa Innovation Foundation. 22 Julai 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-21. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Two Nigerians nominated for AIF innovation awards". guardian.ng. The Guardian Nigeria. 22 Juni 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-21. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Umukoro, Arukaino (2 Julai 2017). "Two Nigerians nominated for Innovation Prize for Africa". punchng.com. The Punch Nigeria. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Omolabake Adenle kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.