Mama wa Mungu wa Vladimir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ilivyo leo.

Mama wa Mungu wa Vladimir ni picha takatifu maarufu ya mtindo wa Eleusa; inamuonyesha Bikira Maria akimpakata mtoto Yesu, nyuso zao zikigusana.[1].

Mchoro asili ulifanywa na msanii asiyejulikana katika karne ya 12, labda Konstantinopoli mwaka 1131. Kutokana na vituko vya historia ulitengenezwa upya mara tano.

Kwa sasa unatunzwa katika Tretyakov Gallery, Moscow, Urusi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. The icon handbook: a guide to understanding icons and the liturgy by David Coomler 1995 ISBN 0-87243-210-6 page 203.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]