Lango:Afrika/Makala iliyochaguliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala iliyochaguliwa[hariri chanzo]

Makala iliyochaguliwa kwa Juni 2012[hariri chanzo]

Jimbo Katoliki la Zanzibar (kwa Kilatini Dioecesis Zanzibarensis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likienea katika visiwa vya Unguja na Pemba vya Tanzania visiwani, jumla kilometa mraba 2,332. Makao makuu yake ni katika mji wa Zanzibar na linahusiana na Jimbo kuu la Dar-es-Salaam. Kanisa kuu limewekwa wakfu kwa heshima ya Mtakatifu Yosefu. Askofu wa jimbo ni Augustine Ndeliakyama Shao, C.S.Sp. Jimbo liliundwa rasmi tarehe 28 Machi 1980 baada ya kujitegemea tangu 12 Desemba 1964 kama Apostolic Administration. Hata hivyo historia ni ndefu zaidi, kwa kuwa tangu mwaka 1860 Zanzibar ilikuwa makao makuu ya Apostolic Vicariate. Waumini ni 9.900 kati ya wakazi 990.900 (sawa na 1%), wengi wao wakiwa Waislamu. Mapadri ni 19, ambao kati yao 15 ni wanajimbo na 4 ni watawa. Hivyo kwa wastani kila mmoja anahudumia waumini 521 katika parokia 7. Mabruda jimboni ni 5, na masista 48.