Kivinje Singino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kivinje Singino ni kata ya Wilaya ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Msimbo wa posta ni 65411.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 32,362 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,376 [2] walioishi humo.

Kata hii inajumlisha mji wa kale Kilwa Kivinje (ndani yake sehemu za Magengeni na Mgongeni) na vijiji vya Singino, Matandu na Nangurukuru.

Singino imepata jina lake kutokana na kilima cha Singino ambako wakati wa ukoloni wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Wajerumani walijenga nyumba ya starehe[3] na mnara mdogo wa kumbukumbu ya chansella Otto von Bismarck[4].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Sensa ya 2012, Lindi - Kilwa DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-04.
  3. picha za kilwa Kivinje pamoja na "Haus des Singino-Verein auf dem Singinoberg bei Kilwa" (nyumba ya klabu ya Singino kwenye kilima cha Singino) na " Singino Vereinshaus, Bismarck-Denkmal" (nyumba ya klabu ya Singino, mnara wa Bismarck)
  4. http://www.bismarcktuerme.de/ebene4/uebers/tansan.html Archived 19 Aprili 2014 at the Wayback Machine. Taarifa ju ya "Bismarckturm" ("mnara wa Bismarck") huko Singino (jer.])
Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania

Chumo | Kandawale | Kibata | Kikole | Kinjumbi | Kipatimu | Kiranjeranje | Kivinje | Lihimalyao | Likawage | Mandawa | Masoko | Miguruwe | Mingumbi | Miteja | Mitole | Namayuni | Nanjirinji | Njinjo | Pande | Somanga | Songosongo | Tingi


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kivinje Singino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.