Federation Aeronautique Internationale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa ndege ya mchezo wa angahewa

Federation Aeronautique Internationale (FAI) ni jina rasmi la Shirikisho la Kimataifa kwa Michezo katika Angahewa. Michezo katika angahewa pamoja na mashindano inaendeshwa kwa kutumia eropleni ndogo za burudani, ndege za nyiririko, parachuti na puto.

Shirikisho hili lilianzishwa mwaka 1905 mjini Paris na makao makuu yapo Lausanne, Uswisi. Shirika inatambuliwa kimataifa kam mtunza wa rekodi katika fani hizi pamoja na usafiri kwenye anga-nje.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]